Thursday, January 24, 2008

MTEGO HUNASA WOTE WALIOKUEMO NA WASIOKUWEMO

Hapo zamani za kale palikuwepo na panya, kuku, , mbuzi na ng’ombe. Panya akawalalamikia wenzake, akaanza na kuku akisema, “Hapa kijijini tulipo kuna mtego unawamaliza panya sisi akina panya tunakwisha, tusaidieni.” Lakini jibu la kuku lilikuwa hivi, “Hilo halinihusu.” Panya hakukata tamaa bali alimwendea mbuzi na kumpa kilio kilekile. Cha ajabu jibu la mbuzi lilikuwa hivi, “sina nafasi na mambo madogo kama hayo.” Panya hakuchoka, alimwendea ng’ombe na kumpa hoja ileile. Jibu la ng’ombe lilikuwa, “Nenda kafie mbali na siku nyingine usinieleze upuuzi kama huo''
Ikafika siku, katika sehemu wanapoishi wote panya, kuku, mbuzi, na ng’ombe, akapita nyoka na kunasa kwenye mtego na kotofanikiwa kutoka. Huku akidhani ni panya, mama mwenye nyumba akapeleka mkono kwenye mtego. Lahaula! Nyoka yule mwenye sumu akamng’ata na mama yule ghafla akaugua sana. Katika kufanya matibabu ikaonekana mgonjwa anahitaji supu na supu ilioonekana nzuri kw mgonjwa ni supu ya kuku. Kuku akachinjwa yuleyule aliyesema mtego haumuhusu. Mama yule hakupata ahueni hivyo akaenda kwenye matibabu ya pesa nyingi. Mbuzi akauzwa ili pesa ipatikane. Aliyemnunua mbuzi ni mchoma nyama na mpika supu, mara baada ya kumnunua alimchinja mbuzi yule kwa ajili ya supu na mishikaki na ni yule yule mbuzi alisema hana nafasi na mambo madogo kama mtego wa panya. Hatimaye mama yule alifariki dunia na watu wengi walikwenda kwenye msiba. Hivyoikaamuriwa ng’ombe achinjwe kwa ajili ya kitoweo. Ng’ombe alichinjwa na ni yuleyule ambaye hataki kuelezwa upuuzi kama mtego wa panya.


JAMANI SAIDIANENI KWENYE SHIDA, RAHA NA MATATIZO.

No comments: